Walioko katika maeneo ya hatari wapewa saa 48 kuhama

  • | K24 Video
    141 views

    Baraza la mawaziri limeagiza wakenya wote wanaoishi ndani ya mifumo dhaifu ya ikolojia inayokabiliwa na mafuriko, maporomoko ya ardhi na kando kando ya mito kuhama katika muda wa saa 48 zijazo. Wakati huohuo wakazi wa Mathare, Ngong na Nairobi kwa jumla watalazimika kuwa ukanda ulio mbali zaidi ya mita 30 kutoka kwa mto uliokaribu kuepuka maafa zaidi.