Waliua vijana bungeni Kenya wafichuliwa

  • | BBC Swahili
    1,704 views
    Mnamo Juni 25, 2024, damu ilimwagika katika Bunge la Kenya. Siku hiyo, maelfu ya waandamanaji walielekea bungeni ili kusitisha muswada wa fedha #FinanceBill2024 kupitishwa kuwa sheria. Njiani walikutana na mabomu ya machozi, virungu, na hata milio ya risasi. Walipofika huko, na kulivamia bunge, baadhi ya milio ya risasi hiyo ikageuka kuwa hatari zaidi Takriban watu watatu waliuawa: mwanafunzi, muuza duka, na mwalimu. Tangu wakati huo, hakuna mtu aliyeshikiliwa kuwajibika kwa vifo vyao. Sasa, #BBCAfricaEye inawafichua walisababisha damu kumwagika nje ya viwanja vya Bunge Kenya. #bbcswahili #financebill #financebill202 Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw