Gavana wa Kaunti ya Kiambu, Kimani Wamatangi, amelaani ubomoaji wa kituo cha elimu ya chekechea katika eneo la Mang’u, Gatundu Kaskazini, kinachodaiwa kubomolewa na mbunge wa eneo hilo jana.Wamatangi alisikitikia tukio la ubomoaji wa kituo hicho cha St. Francis, akilitaja kuwa la kutojali kuhusu kupotea kwa rasilimali za umma zilizotumika kukamilisha mradi huo. Wamatangi amesema hakukuwa na sababu halali ya kubomoa kituo hicho kwa kisingizio cha kutekeleza mradi mwingine wa umma, akiwataka viongozi kukumbatia mashauriano na kutafuta suluhu za amani kwa manufaa ya wananchi.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN
Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#KBCchannel1 #Kenya #News