Wanachama wanne wa baraza la chuo cha Moi watakiwa kufika mbele ya EACC

  • | KBC Video
    6 views

    Kama sehemu ya uchunguzi unaoendelea kuhusu sakata ya ufisadi ya shilingi bilioni 2.2 katika chuo kikuu cha Moi, tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC, imewataka wanachama wanne wa baraza la chuo kikuu hicho kufika mbele yake kuangazia suala hilo. Hatua hiyo ya hivi punde inajiri siku moja tu baada ya naibu chansela wa chuo kikuu cha Moi Isaac Kosgey, kutakiwa kufika katika afisi za EACC kujibu madai ya ubadhirifu kupitia miradi ya miundombinu ambayo imelemaza shughuli katika taasisi hiyo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive