Wanafunzi kutoka Nandi wataka mgao wa basari kuongezwa

  • | Citizen TV
    288 views

    Huku shule na vyuo vikuu vikitarajiwa kufunguliwa wikii hii, wanafunzi wa vyuo vikuu na taaasisi mbalimbali wametaka serikali za ugatuzi kuongeza mgao wa fedha zinazotengwa ufadhili wa masomo. Wakizungumza katika ukumbi wa Eliud Kipchoge mjini kapsabet baada ya kupokea hamasa, wanafunzi hao wameitaka serikali ya kaunti ya Nandi kuongeza mgao wa fedha kutoka shilingi milioni 120 hadi milioni 200 ili kufanikisha elimu.