Wanaharakati akiwemo Boniface Mwangi waachiliwa kwa dhamana

  • | K24 Video
    122 views

    Wanaharakati watano akiwemo Boniface Mwangi wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu ishirini taslimu kila mmoja. Watano hao walifikishwa mahakamani leo baada ya kukamatwa jana na walifunguliwa mashtaka matatu. Wanatuhumiwa kushiriki maandamano kinyume na sheria, kuchapisha taarifa za uongo na uchochezi.