Wananchi watatiza kesi ya kutimuliwa kwa gavana Mwangaza mtandaoni

  • | Citizen TV
    2,465 views

    Kikao cha mahakama cha kusikiza kutimuliwa kwa gavana wa meru kawira mwangaza zimetatizwa baada ya wananchi waliokuwa wakifuatilia kesi hiyo kwa njia ya mtandao kutuma jumbe nyingi na kutatiza. Jaji Bahati Mwamuye aliagiza idadi ya watu wanaohudhuria kesi hiyo kupitia mtandao idhibitiwe ili nidhamu ya mahakama izingatiwe. mahakama imeruhusu kujumuishwa kwa baraza la magavana, FIDA na mpigakura mmoja kutoka kaunti ya Meru katika kesi hiyo. wahusika wametakiwa kuwasilisha stakabadhi na hatikiapo katika siku saba zijazo huku kesi ikipangiwa kuanza tarehe 8 oktoba. gavana Kawira Mwangaza anapinga uamuzi wa bunge la seneti lililoafikia kumwondoa ofisini baada ya bunge la kaunti ya meru kufanya hivyo.