Wanawake kuhusishwa katika kutafuta suluhu za amani na usalama Afrika

  • | VOA Swahili
    59 views
    Dunia inapoadhimisha siku 16 kupinga ukatili wa kijinsia, mataifa wanachama wa shirika la Maendeleo ya serikali za mataifa ya Upembe wa Afrika IGAD, yamekubaliana kutekeleza sera ya pamoja ya kuhusisha wanawake katika kukabiliana na mizozo inayoathiri Amani na usalama. IGAD inasema changamoto za kiusalama katika mataifa mwanachama wake zinawiana, na kwamba mkakati wa mwaka 2023 hadi 2030 kuhusisha wanawake katika kutafuta suluhu la Amani na usalama ndio njia ya suluhu. #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.