- 271 viewsDuration: 2:20Muungano wa watawa wa kanisa katoliki nchini unaitaka serikali pamoja na mashirika ya kijamii kuweka mikakati maalum ya kulinda watoto kutokana na ongezeko la visa vya ulanguzi wa kingono miongoni mwa watoto hasa katika maeneo ya ukanda wa pwani. Wakizungumza mjini Kilifi baada ya warsha iliyowaleta pamoja wadau mbali mbali yakiwemo mashirika ya kijamii watawa hao wamesema kuwa ipo haja ya kuanzishwa kwa kampeini yakuhamasisha wazazi kuhusu madhara ya ulanguzi huo huku wakitaja mikahawa, fuo za bahari na nyumba za kukodi maarufu kama AirBnB kuwa maeneo yanayotumiwa kutekeleza dhulma dhidi ya watoto. Mashirika ya kijamii pamoja na muungano huo sasa wameanzisha mchakato wa kushinikiza jamii pamoja na serikali kulinda watoto kutokana na jinamizi hilo huku msimu wa likizo ndefu ukikaribia.