Watu 11 wafariki Bukavu kwa mkutano wa M23

  • | BBC Swahili
    1,839 views
    Watu kumi na mmoja wamethibitishwa kufariki baada ya milipuko miwili kutokea katika mji wa Bukavu, mashariki mwa DRC leo siku ya Alhamisi, punde tu baada ya mkutano wa M23 uliohudhuriwa na mmoja wa viongozi wa kundi hilo la waasi Corneille Nangaa katika uwanja wa Independent Square. Mlipuko wa kwanza ulisababisha hali ya sintofahamu na kuwalazimisha watu kutawanyika kabla ya mlipuko wa pili. Wakazi waliwasaidia waliojeruhiwa. Bukavu ni moja wapo ya miji mikuu katika eneo hilo iliyotekwa katika majuma ya hivi karibuni na wapiganani wa M23 ambao umoja wa mataifa umesema wanaungwa mkono na Rwanda. Nangaa alikuwa ameondoka katika uwanja huo ambako mkutano huo ulifanyika. M23 walidhibiti mji wa Bukavu baada ya kuteka Goma ambao ni mji mkuu wa Kivu Kaskazini.