Watu wanne wafariki Kamkunji baada ya bomba la maji taka lililokuwa likikarabatiwa kuporomoka

  • | K24 Video
    98 views

    Watu wanne wamefariki katika eneo la shauri moyo, huko kamkunji baada ya bomba la maji taka lililokuwa likikarabatiwa kuporomoka na kufunika watu saba, usiku wa manane. Hata hivyo watu watatu kati yao walinusurika kifo na wanauguzwa majeraha. Wakazi wa eneo hilo wameghadhabishwa na tukio hilo wakidai kuwa mkandarasi hakufuata sheria za ujenzi mbali na kuamua kufanya kazi hiyo usiku. Isitoshe baadhi ya wakaazi wanadai kuwa huenda zaidi ya watu saba bado wamefunikwa na mchanga, wakiwataka maafisa wa polisi kuwaruhusu wachimbe.