Watu watatu wafariki kwenye ajali ya barabarani Nanyuki

  • | KBC Video
    160 views

    Watu watatu walifariki huku mwingine akijeruhiwa vibaya kufuatia ajali kwenye barabara kuu ya kutoka Meru kuelekea Nanyuki. Ajali hiyo ilijiri baada ya trela lililokuwa limebeba lori kupoteza mwelekeo na kuanguka eneo la Maili saba. Kulingana na walioshuhudia, ajali hiyo inadaiwa kuchangiwa na mteremko unaofululiza kutoka makutano ya Subuiga hadi mahali ajali ilipotukia. Wakazi wa eneo hilo wametoa wito kwa serikali kutangaza eneo hilo kuwa hatari kutokana na ajali nyingi zinazoshuhudiwa. Mtu aliyejeruhiwa anapokea matibabu katika hospitali ya matibabu maalum ya Isiolo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive