Watu watatu wakamatwa kwa uendeshaji mbaya wa gari kwenye barabara ya Kenol-Sagana

  • | Citizen TV
    2,015 views

    Watu watatu walionaswa wakiendesha gari kiholela wamekamatwa na wanafikishwa mahakamani kaunti ya Murang'a Katika kanda ya video iliyosambazwa kwenye mitandao, madereva wa magari haya walionekana wakiendesha matatu vibaya, huku baadhi ya abiria wakiwa wananing'inia kwenye madirisha. Tukio hili lilinaswa katika eneo la Makuyu kwenye barabara ya Kenol kuelekea Sagana. Miongoni mwa waliokamatwa ni mwenye gari moja, mwanawe ambaye ndiye alikuwa kondakta siku hiyo na dereva. Mshirikishi wa maswala ya trafiki eneo la Kati Elizabeth Vivi amewarai madereva kuwajibika