Wauguzi wa Machakos wasusia kazi

  • | Citizen TV
    289 views

    Wauguzi hao wanasema kuwa kwa miezi mitatu sasa wameshindwa kulipia mikopo kutokana na kucheleweshwa kwa mshahara. Wakizungumza katika hospitali ya Machakos Level 5, wauguzi hao wamesema hawatafanya kazi hadi pale serikali ya kaunti itakaposkiza kilio chao.Kaunti ya Machakos ina takriban wauguzi 1,350 ambao pia wanadai kunyanyaswa na usimamizi wa hospitali hiyo wakidai kushurutishwa kufanya kazi kwa saa 160.