Wazee na viongozi wa makanisa wafanya kikao Kisii kujitayarisha kwa ziara ya rais

  • | Citizen TV
    2,648 views

    Wazee wa jamii ya Abagusii pamoja na wenzao wa makanisa wamerai viongozi wa kaunti ya Kisii kuzungumza kwa sauti moja katika kikao wanachotarajia kuwa nacho na Rais William Ruto atakapozuru eneo hilo kesho. Wakizungumza mjini Kisii, wazee hao wametoa wito kwa waliochaguliwa kote Kisii kuweka tofauti zao kando kwa manufaa ya wakazi ili miradi iliyoanzishwa ya maendeleo na kuboreshwa kwa miundo msingi ikamilishwe.