Wazee wa Kaya Kwale wataka misitu ya Kaya kulindwa

  • | Citizen TV
    137 views

    Wazee wa Kaya kaunti ya Kwale wameitaka serikali kujumuisha uokoaji wa misitu ya Kaya inayonyakuliwa kwenye mpango wa kufidia wamiliki wa mashamba wasioyatumia kwa minajili ya kuwapa wenyeji ardhi. Wazee hao wamesema mpango huo uliotangazwa na Rais William Ruto wakati wa sherehe za Mashujaa mwaka jana, utasaidia pakubwa kuhifadhi misitu ya Kaya iwapo wanaodai uimiliki watalipwa na kuiondokea.