Waziri Aden Duale asema wafisadi wamejaa ndani ya wizara ya afya

  • | Citizen TV
    1,864 views

    Waziri wa Afya Aden Duale ametambua kuwepo kwa makundi ya wafidsadi katika wizara hiyo ambao wamekwamisha utoaji wa huduma bora za afya kwa miaka mingi. Duale sasa ameapa kusafisha wizara hiyo na kurejesha utaratibu. Anapojitayarisha kuchukua rasmi mamlaka Jumanne, Duale anasema yuko tayari kwa kazi na jukumu la kwanza litakuwa kuhakiki madeni ya bima ya afya ya zamani NHIF.