Waziri Murkomen aitetea wizara yake na idara ya polisi kwa kazi inayofanya.

  • | K24 Video
    77 views

    Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen ameitetea wizara yake na idara ya polisi kwa kazi inayofanya. Utetezi huo umefuatia kusolewa vikali na baadhi ya wanasiasa na vyombo vya habari kutokana na visa vya uhalifu nchini. isitoshe ametoa changamoto kwa wanaomshtuhumu kuzuru maeneo yaliyokumbwa na uhalifu ili kushuhudia utendakazi wa maafisa wa polisi. ijapokuwa alitetea operesheni za kudhibiti uhalifu maeneo ya Baringo, Murkomen hakuzungumiza shambulio la kigaidi lililoua maafisa sita wa polisi huko Garrisa.