Skip to main content
Skip to main content

Waziri wa AI atambulishwa bungeni-Albania

  • | BBC Swahili
    12,027 views
    Duration: 1:06
    Waziri Mkuu wa Albania amemtambulisha “waziri wa AI” kwa wabunge bungeni. Waziri Mkuu Edi Rama alimtangaza Diella kama sehemu ya baraza lake jipya la mawaziri siku chache zilizopita, akimkabidhi jukumu la kusimamia ununuzi wa umma na kupambana na ufisadi wa muda mrefu. Alisema jukumu lake litakuwa kuhakikisha Albania inakuwa “nchi ambayo zabuni za umma ni huru kwa asilimia 100 bila kuingiliwa na mafisadi.” Katiba ya Albania inasisitiza kuwa mawaziri lazima wawe raia wenye akili timamu na walio na umri wa angalau miaka 18. Chama cha upinzani cha Democratic Party kimeita hatua hiyo “ya kipuuzi” na “kinyume cha katiba.” 🎥: @frankmavura - - #bbcswahili #akilimnembe #uongozi #siasa