Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza Wasaini Mkataba wa Hifadhi

  • | VOA Swahili
    252 views
    Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza James Cleverly na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Vincent Biruta wamesaini mkataba wa hifadhi katika juhudi za kuufufua mpango wa pamoja wa serikali kuwahamisha wahamiaji kwenda katika taifa la Afrika Mashariki. Mkataba mpya ni matokeo ya ziara ya Cleverly nchini Rwanda Jumanne, ambako alikutana na Biruta na kusaini mkataba kwa matumaini ya kukabiliana na uamuzi wa Mahakama ya Juu uliopitishwa mwezi uliopita ambao ulisema mpango huo ni kinyume cha sheria. “Rwanda hivi sasa imekuwa na sifa thabiti ya kujali wengine na weledi wa usimamizi wa wakimbizi na wahamiaji,” Cleverly alisema wakati wa kusaini mkataba huo. (VOA) #britain #rwanda #asylum #treaty #africa #voa