Wizara ya afya yasisitiza uwajibikaji kuhusu mamlaka ya afya ya SHA

  • | K24 Video
    42 views

    Wizara ya afya imesisitiza uwajibikaji kuhusu mamlaka ya afya ya jamii (SHA), huku waziri wa afya, Debora Barasa, akisema kuwa wizara iko tayari kufika mbele ya kamati yoyote kujibu maswali, ikiwemo ripoti ya mkaguzi mkuu wa mahesabu serikalini kuhusu ukiukwaji wa ununuzi wa mfumo wa teknolojia wa SHA. Wakati huo huo, viongozi wa kanisa wametoa wito kwa serikali kuharakisha juhudi za kurekebisha changamoto zinazokumba SHA.