Yuko wapi ezekiel machuki : Familia yadai haki baada ya mpendwa wao kutoweka

  • | KBC Video
    27 views

    Familia moja katika kaunti ya Kisii inasononeka kufuatia kutoweka kwa jamaa wao kwa njia ambayo haieleweki. Ezekiel Machuki, aliyekuwa mhudumu wa Boda Boda, alitoweka mwezi Novemba mwaka jana. Mamaye Machuki anadai kwamba afisa wa kikosi cha ulinzi cha Kenya, ambaye pia alikuwa rafikiye, anaweza kuwa na taarifa kuhusu aliko baada kumwitisha Ezekiel shilingi laki-4 akiahidi kumsaidia kupata kazi katika jeshi. Kesi hiyo iliripotiwa kwa utawala, na afisa huyo akahojiwa na idara ya upelelezi wa jinai lakini Machuki bado hajapatikana. Familia hiyo sasa inaomba msaada ili kumpata jamaa wao.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive