Zaidi ya nyumba 300 zimeteketea eneo la Soweto Kibra

  • | Citizen TV
    13,047 views

    Zaidi ya nyumba mia tatu zimeteketea katika eneo la Soweto mtaani Kibra. Polisi wangali wanachunguza chanzo cha moto huo ingawa inadaiwa kuwa ulisababishwa na hitilafu za nguvu za umeme. Inaarifiwa kuwa moto huo ulianzia kwenye nyumba moja na kisha kusambaa kwa kasi kwasababu wazimamoto walichelewa kufika.watu kadhaa walijeruhiwa huku mali ya thamani isiyojulikana ikiteketea.