Familia ya mfanyabiashara Bunty Bharat Shah, ambaye inaripotiwa aliuawa na maafisa wa polisi waliokuwa wamejifunika nyuso nyumbani kwake mtaani Westlands mwaka 2017, sasa inadai malipo ya fidia yanayozidi shilingi milioni 700. Kupitia kwa wakili mkuu Ahmednasir Abdullahi, jaji wa mahakama kuu Chacha Mwita aliarifiwa kuwa maisha ya marehemu yalikatizwa, na hivyo kunyimwa haki ya kuishi kama ilivyoainishwa katika Katiba. Mnamo tarehe 12 mwezi Septemba mwaka huu, mahakama ya rufani ilitangaza kuwa mauaji ya aliyekuwa mkurugenzi wa kampuni ya Bobmil, Bunty Bharat Shah, yaliyotekelezwa na maafisa wa polisi waliokuwa wamejifunika nyuso, yalikuwa kinyume cha sheria. Jaji Chacha Mwita alitangaza tarehe 20 mwezi Machi mwaka ujao kuwa siku ya kutolewa kwa hukumu ya kesi hiyo.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive