Skip to main content
Skip to main content

Hatua madhubuti za trafiki zimetangazwa kufuatia ongezeko la ajali barabarani

  • | KBC Video
    3,127 views
    Duration: 4:33
    Baraza la kitaifa linaloshughulikia utekelezaji wa haki limetangaza hatua madhubuti za trafiki kufuatia kuongezeka kwa ajali za barabarani nchini, huku shughuli za usafiri zikiongezeka msimu huu wa sherehe. Wakikutana katika mahakama ya upeo, jaji mkuu Martha Koome, pamoja na maafisa wa idara ya polisi, waendesha mashtaka, wadhibiti wa sekta ya uchukuzi pamoja na mashirika ya kukabiliana na ufisadi walitangaza mbinu shirikishi itakayotumika katika juhudi za kupunguza ajali hizo msimu huu na hata baadaye. Haya yanajiri huku takwimu rasmi zikionesha ongezeko la asilimia tano katika vifo vinavyohusiana na ukiukaji wa kanuni za trafiki mwaka huu. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #KBCchannel1 #Kenya #News