Skip to main content
Skip to main content

Mwandishi mahiri wa BBC Jamhuri Mwavyombo astaafu

  • | BBC Swahili
    14,180 views
    Duration: 7:02
    Baada ya miaka 25 ya kazi kuntu hapa BBC, Jamhuri Mwavyombo au Sister J, kama wengi wetu tunavyomfahamu anastaafu rasmi. Safari yake ndani ya BBC imejaa historia ya kipekee: kuanzia siku zake katika BBC World Service Trust, ambayo sasa inajulikana kama BBC Media Action, hadi kazi yake yenye uzito kama mwandishi wetu jijini Arusha, Tanzania akiripoti kuhusu Mahakama ya Kimataifa ya Rwanda, chombo cha Umoja wa Mataifa kilichoshughulikia wahusika wa mauaji ya kimbari ya 1994. Baadaye, alihamia katika ofisi zetu za hapa Nairobi ambapo mchango wake uliendelea kujidhihirisha ubora wake wa uandishi, weledi na hekima. #DiraYaDuniaTV