Skip to main content
Skip to main content

Rais Trump kuongoza makubaliano ya amani kati ya DRC na Rwanda

  • | BBC Swahili
    1,329 views
    Duration: 4:21
    Rais wa Marekani Donald Trump , hii leo ni mwenyeji wa viongozi wakuu kutoka Rwanda na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambao wanatarajiwa kutia Saini mkataba wa amani ambao unatarajiwa kuleta amani ya kudumu katika eneo la Mashariki mwa DRC ambalo limekumbwa na mapigano kwa zaidi ya miongo mitatu. Kikao cha leo ni cha pili kuandaliwa Marekani baada ya Mawaziri wa kigeni wa mataifa hayo mawili kutia saini mkataba wa makubaliano mnamo Juni mwaka huu, katika kikao kilichosimamiwa na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio. Leila Mohammed @mrs.tadicha anafafanua masuala kuu yaliyoafikiwa wakati huo huku wengi wakasubiria kujua ni yapi mampya ambayo yatajitokeza kwenye kikao cha leo. - - #bbcswahili #trump #drc #rwanda #m23