Skip to main content
Skip to main content

Tazama daraja likiporomoka China

  • | BBC Swahili
    10,104 views
    Duration: 51s
    Daraja jipya lililofunguliwa hivi karibuni katika jimbo la Sichuan, kusini magharibi mwa China, upande mmoja umeporomoka na kusababisha wingu kubwa la vumbi. Mamlaka zilifunga daraja la Hongqi lenye urefu wa mita 758 (futi 2,486) siku ya Jumatatu baada ya nyufa kuonekana kwenye barabara zilizo karibu. Jumanne mchana, hali katika eneo la mlima ilizidi kuwa mbaya na kusababisha maporomoko ya ardhi yaliyosababisha sehemu ya daraja hilo kuporomoka, maafisa walisema. Hakukuripotiwa vifo au majeruhi. Ujenzi wa daraja hilo ulikamilika mapema mwaka huu, kwa mujibu wa chapisho la mitandao ya kijamii kutoka kwa wakandarasi wa Sichuan Road and Bridge Group. - - #bbcswahili #China #miundombinu #ajali Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw