- 872 viewsDuration: 2:04Chama cha usalama wa bodaboda nchini, viongozi wa wahudumu wa bodaboda pamoja na wakuu wa polisi wamekutana kujadili mikakati ya kukabiliana na uhalifu wa baadhi ya wanabodaboda hasa wanaoteketeza magari panapotokea ajali. Imeafikiwa kuwa kila mhudumu wa bodaboda ni sharti ajiunge na sacco, huku pendekezo likitolewa kwamba wahudumu wavalie sare maalum kulingana na kaunti zao miongoni mwa mapendekezo mengine.