- 402 viewsDuration: 2:24Wanasayansi wanaendeleza uzalishaji wa viazi vya kisaki au vile ambavyo vimeboreshwa kijenetiki ili kuwapunguzia wakulima wa viazi gharama inayosababishwa na ugonjwa wa kuvu. Shirika la Utafiti wa Kilimo na Mifugo (KALRO) huko Muguga, kaunti ya Kiambu linaendeleza kilimo cha viazi vilivyo na uwezo wa kustahimili ugonjwa wa kuvu. Kilimo hicho kinapania kuwaongezea wakulima mazao na mapato, kama anavyoarifu Denis Otieno kwenye makala ya leo ya Kilimo Biashara.