Skip to main content
Skip to main content

Mbu werevu wanaokwepa vyandarua

  • | BBC Swahili
    4,166 views
    Duration: 1:34
    Wakenya wako katika hatari kubwa ya maambukizi ya malaria kutokana na mbu aina ya Anopheles funestus kubadilika kitabia na kijenetiki. Utafiti mpya umeonyesha kuwa mbu hawa sasa wanakwepa vyandarua kwa kuuma mchana wakiwa nje na pia wameanza kustahimili viua-viwadudu. Utafiti huu uliohusisha taasisi ya KEMRI, watafiti kutoka nchi 13 za Afrika, na Wellcome Sanger Institute, ulifuatilia zaidi ya jenomu 650 za mbu – hata kutoka miaka ya 1920 – na kubaini kuwa usugu dhidi ya dawa umekuwepo kwa miongo kadhaa. Mwandishi wa BBC @frankmavura na taarifa kamili juu ya utafiti huo. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw