Tanzania yaanzisha mfumo wa kidigitali katika sekta ya madini

  • | VOA Swahili
    426 views
    Akizungumza na Sauti ya Amerika, Nicholaus Kaserwa, Afisa Mwandamizi wa Uendeshaji Biashara wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), alisema kuwa mfumo huo wa kidijitali umeanzishwa na serikali kwa lengo la kurahisisha ununuzi na uuzaji wa madini. "Katika sekta ya madini, maboresho yanakuja kupitia mnada wa mtandao. Madini yanachambuliwa, kuwekwa kwenye mafungu ya lot, na kutengeneza katalogi ambayo inawasilishwa kwa wanunuzi. Wanunuzi huipitia, kuchagua wanachotaka kuona, na hatimaye kuweka bei zao kupitia mfumo wa kidijitali," alisema Kaserwa. #tanzania #mfumo #kidigitali #madini #ununuzi #uuzaji #sokolabidhaa #nicholauskaserwa #mererani #manyara #mkoa #voa #voaswahili