Mfanyabiashara wa Tanzanite apongeza fursa ya kununua madini moja kwa moja

  • | VOA Swahili
    437 views
    Switi Nkiya, mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite, alieleza kuwa mfumo wa sasa wa kidigitali katika sekta ya madini umewanufaisha zaidi wafanyabiashara wakubwa kwa sababu wanamitaji mikubwa kuliko wadogo. "Ni muhimu serikali itutenganishe ili kuhakikisha kila mmoja anapata nafasi sawa ya kunufaika," alisema Nkiya. Lakini amepongeza hatua ya serikali kutoa fursa kwa wafanyabiashara wadogo kununua madini moja kwa moja. Katika sekta ya madini, Nicholaus Kaserwa, Afisa Mwandamizi wa Uendeshaji Biashara wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), amesema maboresho yanakuja kupitia mnada wa mtandao. Madini yanachambuliwa, kuwekwa kwenye mafungu ya lot, na kutengeneza katalogi ambayo inawasilishwa kwa wanunuzi. Wanunuzi huipitia, kuchagua wanachotaka kuona, na hatimaye kuweka bei zao kupitia mfumo wa kidijitali," alisema Kaserwa.⁣ Sikiliza ripoti kamili iliyoandaliwa na mwandishi wa VOA, Amri Ramadhani, Mkoa wa Manyara, Tanzania. #tanzania #mfumo #kidigitali #madini #ununuzi #uuzaji #sokolabidhaa #nicholauskaserwa #mererani #manyara #mkoa #voa #voaswahili