- 528 viewsKatika eneo linalopambana na changamoto za afya na kukumbwa na vita, waandishi wa kubaini habari za uongo katika jarida la Eleza ukweli mjini Goma, DRC, wanatafuta habari za ukweli kuhusu fikra zinazoambatana na ugonjwa mpox ambao awali ulikuwa unajulikana kama ugonjwa kutoka kwa nyani. Habari za uongo zinasema kwamba ugonjwa huo haupo kabisa na kwamba yanayosemwa ni upele tu ambao hauna madhara. Aline Kataliko anasema kazi yao ni muhimu sana kwa afya ya umma na katika kujenga imani katika jamii. Aline Kataliko wa Eleza Fact: 'Kuna uvumi kuhusu mpox, unaosema kwamba lengo la chanjo ni kuondoa kizazi cha raia wa Congo. Tunaangazia hatari za uvumi huo na namna unavyoweza kuathiri jamii yote kwa jumla na kuzuia juhudi za kumaliza maambukizi." Tangu mwaka 2021, waandishi wa habari 25 katika jarida la Eleza ukweli, akiwemo Joel Alimasi Kitambala, wamekuwa wakiangazia na kueneza habari kuhusu hatari za habari potofu. Joel Alimasi Kitambala ni mwandishi wa habari katika Eleza Ukweli. Joel Alimasi Kitambala wa Eleza Fact: Kutambua ukweli, tunatumia maneno muhimu na kila wakati kuna chapisho ambalo lina maneno hayo, tunapata taarifa kuhusu chapisho hilo. Kama kuna hja ya kuchambua jarida hilo, waandishi wa kutafuta ukweli wanapewa jukumu wanaolifanyia kazi. Makala yanayochapishwa na Eleza ukweli, yanachapishwa kwenye wavuti, na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kutangazwa kwenye vituo vya radio ili kuwafikia wale wasiotumia internet. #habaripotofu #drc #goma #waandishi #voa #voaswahili
Habari potofu kuhusu chanjo kuondoa kizazi na athari kwa jamii
- - 2025 SOYA Awards ››
- - 🔴 LIVE || TV47 ››
- 19 Apr 2025 - Canada's Prime Minister Mark Carney faced sustained attacks from his Conservative rival at an election debate Thursday, but the Liberal leader sought to focus attention on what he calls Canada's top threat, President Donald Trump.
- 19 Apr 2025 - Iran staged military parades on Friday to mark its annual Army Day celebrations, showcasing a wide array of its latest domestically built drones, missiles, tanks, and other hardware.
- 19 Apr 2025 - Top county officials summoned in waste firm deal
- 19 Apr 2025 - A woman is in custody after being found in possession of nearly 300 grams of cocaine, following a sting by a multi-agency security team targeting drug trafficking routes between Kenya’s Northern Frontier and the capital.
- 19 Apr 2025 - Idriss noted that the agency has observed a significant shift from development aid to investment-based financing, helping narrow the funding gap for well-prepared infrastructure projects.
- 19 Apr 2025 - After a 14-month hiatus, former Interior CS Fred Matiang'i, who left the country under a cloud of controversy after his home was raided by police, is back in the public sphere.
- 18 Apr 2025 - Detectives at the Kayole Police Station in Nairobi are holding a senior Imam for the offence of causing grievous harm to at least two persons.
- 18 Apr 2025 - Gas blast kills two, injures several in Embakasi South
- 18 Apr 2025 - Managing leg disorders in broiler chickens
- 18 Apr 2025 - Chaos erupted at the Kitale Museum on Friday afternoon as a modelling competition was violently disrupted by over 50 armed youths.