Mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi afichua kwamba wanawake 100 waliuawa kati ya Agosti na Novemba

  • | K24 Video
    22 views

    Mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi amefichua kwamba wanawake 100 waliuawa kati ya Agosti na Novemba 2024. Mudavadi, ambaye pia ni kaimu waziri wa usalama wa ndani, amesema mauaji ya wanawake ni tatizo kubwa linalokumba sekta ya usalama. Mudavadi vilevile ameeleza kuwa kenya imerekodi jumla ya visa 7,107 vya ukatili wa kijinsia kati ya septemba mwaka jana na mwezi huu.