- 85 viewsKwa kuenea kwa taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii, waandishi wa habari nchini Msumbiji wako mstari wa mbele katika kupambana na upotoshaji na taarifa za uongo. Hapa katika chumba cha habari cha Evidencias, mjini Maputo, Msumbiji, Reginaldo Tchambule na timu yake wanafanya kazi ya kuweka rekodi sawa katika jitihada za kupambana na upotoshaji na taarifa za uongo. Yeye na mwenzake Nelson Mucandze, wanasema walianzisha pamoja gazeti na lile la mtandaoni miaka minne iliyopita kwa sababu mashirika mengine mengi hayakuwa yakikagua ukweli au kutumia taarifa na uchambuzi katika kuripoti kwao. Tchambule anasema hadhira yao ilianza kufuatilia kwa haraka. Reginaldo Tchambule, Evidencias Editor anaeleza: “Gazeti la Evidencias linaweza kuwa limepata muonekano na umaarufu mkubwa katika muda mfupi, kwa sababu ya jinsi tulivyozingatia uandishi wa habari wenyewe. Wakati fulani tulikuwa na ukurasa ambapo tulichunguza habari kuu zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.” Mwaka huu, Tchambule aliripoti kwa nini Ossufo Momade, kiongozi wa Renamo, chama kikuu cha upinzani cha Msumbiji, hajaonekana hadharani kwa wiki kadhaa wakati wa kampeni za urais. Evidencias ilianza kuchunguza picha kwenye mtandao wa Facebook wa mgombea ambapo ilionekana Momade alikuwa akifanya kazi nje ya nchi. Ripoti ya Amarilis Gule VOA Maputo. #habaripotofu #msumbiji #maputo #chumbachahabari #Evidencias #gazeti #reginaldotchambule #voa #voaswahili
Nchini Msumbiji waandishi waongeza juhudi kukabiliana na habari potofu
- 24 Dec 2024 - It is now emerging that a large percentage of Kenyans may be suffering from diseases they are unaware of.
- 24 Dec 2024 - Counterfeiting is a significant and growing problem globally, particularly in low-income economies like Kenya.
- 24 Dec 2024 - President William Ruto on Tuesday met African Union Commission (AUC) chairperson Moussa Faki to hold talks on implement reforms at the African Union.
- 24 Dec 2024 - At least 207 people were killed by members of the Wharf Jeremie gang in Haiti's portside neighborhood of Cite Soleil earlier this month, the United Nations said in a report on Monday, revising a death toll it initially estimated at 187.
- 24 Dec 2024 - This comes as speculations continue on whether Gachagua will join the opposition.
- 24 Dec 2024 - When he came to Kenya at the start of 2023, Yuto Kusaba had harbored a dream of playing professional football back at home in Japan, laying his sights on the J League and ultimately, the nat…
- 24 Dec 2024 - Former President Bill Clinton was admitted Monday to MedStar Georgetown University Hospital in Washington after developing a fever.
- 24 Dec 2024 - Their talks focused on the upcoming election for the AUC chairperson
- 24 Dec 2024 - CS Duale joins the list of senior government officials who have come out to slam Gachagua over his remarks.
- 24 Dec 2024 - Climate WorX initiative addresses climate challenges through community-driven solutions.