Mhariri wa Kituo cha DMRTV aeleza jinsi habari potofu zilivyo enezwa katika soka

  • | VOA Swahili
    187 views
    Jude Mbaku ni mwanahabari mwingine, na mhariri mkuu wa DMRTV Buea, mkaguzi mkuu wa kuhakiki habari za kweli katika eneo ambalo hapo awali liliathiriwa na habari potofu. Mbaku anasema ameona makundi yanayotumia mitandao ya kijamii kupotosha umma, na matokeo yake ni makubwa. Jude Mbaku wa DMRTV Buea -Mhariri Mkuu anasema: Timu ya Cameroon ilipokwenda Cote d’Ivoire kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, tetesi zilienea kwamba Njie Clinton amejiuzulu kwenye kikosi. Na walioeneza habari hizi walikuwa wapiganaji waliojitenga. Hili halikufanywa kama jambo la makosa. Ilikuwa imeandaliwa vizuri na kutayarishwa vyema ili kupotosha watu. Karloff anasema kuwa waandishi wa habari wa Cameroon wanakabiliwa na changamoto nyingi katika kuripoti kwa usahihi, ikiwa ni pamoja na ufadhili mdogo, hatari za usalama, na upatikanaji mdogo wa habari. Boris-Kaloff Meneja wa kituo cha CBS Buea anatoa maelezo zaidi: "Nchini Cameroon, ni vigumu kupata takwimu na data. Unajua, nimekwenda kwa wajumbe wa kanda wa usafiri kuulizia takwimu za magari yaliyosajiliwa kusini-magharibi, haswa huko Buea, na nikaambiwa niende kusimama barabarani kuanza kuhesabu magari mimi mwenyewe." Ripoti ya Njodzeka Danhatu wa VOA, Buea, Cameroon. #timu #mpira #cameroon #voa #voaswahili #njieclinton #cotedivoire #judembaku #dmrtvbuea #mharirimkuu #voa #voaswahili #habaripotofu