Waziri wa elimu atangaza matokeo ya KCSE 2024

  • | KBC Video
    3,346 views

    MATOKEO YA MTIHANI WA KCSE 2024

    Baraza la kitaifa la mitihani nchini limetangaza matokeo ya mtihani wa KCSE mwaka 2024 yaliyoonyesha kuimarika kwa matokeo ya watahiniwa ikilinganishwa na mwaka 2023. Kwenye matokeo hayo jumla ya watahiniwa 1,693 walipata alama ya A hili likiwa ongezeko la watahiniwa 477 ikilinganishwa na mwaka 2023 huku watahiniwa 246,391 wakifuzu kujiunga na chuo kikuu bada ya kupata alama ya C+ na zaidi. Kadhalika wizara ya elimu imetangaza kuanzishwa kwa mtihani wa kitaifa wa KCSE wa katikati ya mwaka utakaoandaliwa mwezi Julai ili kuwashughulikia wanafunzi wanaokabiliwa na chamgamoto kufanya mtihani wa mwisho wa mwaka. Mwanahabari wetu Joseph Wakhungu anatuarifu zaidi kuhusu matokeo ya mtihani wa KCSE wa mwaka 2024.

    #Darubini

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive