Moto wa msituni uliyoleta maafa umewaacha maelfu bila ya makaazi

  • | VOA Swahili
    214 views
    Moto wa msituni uliendelea kuwaka katika eneo lote la kifahari la Los Angeles Januari 7, na kuharibu nyumba na kusababisha msongamano wa magari barabarani wakati watu 30,000 walipokuwa wakiondoka huku wamefunikwa na moshi mkubwa ambao uko katika sehemu kubwa ya mji huo. Ekari zisizopungua 1,262 za eneo la Pacific Palisades lililoko kati ya Santa Monica na Malibu liliungua, maafisa walisema, baada ya kuwa tayari wametahadharisha kuwepo moto wenye hatari kubwa kutokana na upepo wenye nguvu uliokuwa ukipiga eneo hilo kutokana na kipindi cha hali ya hewa yenye mimea iliyokauka. Moto huo ulienea kwa kasi kwa kipindi cha saa chache wakati maafisa wakitahadharisha kuwepo hali ya upepo mkali iliyotarajiwa kutokea usiku kucha, ikipelekea wasiwasi kuwa maeneo jirani mengi zaidi yangeweza kulazimika kukimbia maeneo yao. #marekani #la #wildfires #voaswahili #santamonica #malibu #makazi #california #losangeles