SHA: Spika aitaka kamati ya afya kuandaa kikao

  • | Citizen TV
    318 views

    Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula ameiagiza kamati ya afya bungeni kuandaa kikao na wadau wote wa sekta ya afya kuzungumzia changamoto zinazoibuka kuhusiana na mpango wa bima ya afya sha. Akizungumza katika eneo la Khwisero, kaunti ya Kakamega, wetangula ametaka mkutano huo kutafuta suluhu ya changamoto zinazowafanya wakenya kukosa huduma za afya licha ya kulipia bima hiyo.