Muturi: Wakenya wanataka kujua ukweli kuhusu utekaji nyara

  • | KBC Video
    137 views

    Waziri wa utumishi wa umma Justin Muturi anapendekeza kubuniwa kwa tume ya uchunguzi kushughulikia kile anachotaja kuwa kuongezeka kwa visa vya utekaji nyara na mauaji humu nchini. Akizungumza baada ya kuzuru makafani ya City kufariji familia zinazowatafuta jamaa wao waliotoweka, Muturi alisema Wakenya wanahitaji kujua ni nani aliyehusika na utekaji nyara huo. Matamshi hayo yanajiri huku spika wa bunge la taifa Moses Wetangula akitoa wito wa uchunguzi wa kina kuhusu madai ya utekaji nyara.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive