Familia yalilia haki baada ya mwanao kuuawa kwa kudungwa kisu kanisani

  • | Citizen TV
    2,029 views

    Familia moja kutoka kaunti ya Homa Bay inadai haki baada ya jamaa yao kuuwawa ndani ya kanisa. Francis Opiyo aliuwawa kwa kudungwa kisu kifuani Jumamosi, akijitayarisha kufanya matangazo katika kanisa la Ebenezer Adventist eneo la Suba. Na kama anavyoarifu Laura Otieno, mshukiwa mkuu wa mauaji hayo anadaiwa kuwa na mzozo wa kimapenzi na Opiyo ambaye alikuwa mmoja wa viongozi wa kanisa hilo.