Vijana kutoka Ethiopia wavuka mpaka kazi Kenya

  • | Citizen TV
    4,574 views

    Ukosefu wa ajira ukionekana kuzima azma ya vijana wengi humu nchini na kuwalazimu baadhi kusafiri ughaibuni kutafuta kazi, kinaya ni kuwa hali ni tofauti katika eneo la Moyale mpakani mwa Kenya na Ethiopia. Hii ni kwa kuwa vijana kutoka taifa la Ethiopia, huvuka mpaka kila siku kuingia Kenya kujitafutia kazi.