Gavana Patrick Ole Ntutu ataka wasichana kuelimishwa

  • | Citizen TV
    184 views

    Gavana wa Narok Patrick Ole Ntutu amewahimiza wazazi wa eneo hilo kuhakikisha kuwa watoto wa kike wanapata elimu kama wenzao wa kiume. Akizungumza katika shule ya upili ya Olderkesi, Gavana Ntutu akisema kuwa ni muhimu kwa wazazi kuwapa nafasi sawa ya elimu watoto wote akionya dhidi ya kuongezeka kwa mimba za utotoni. Shule ya Olderkesi iliongoza kaunti katika mtihani wa kidato cha nne mwaka jana ambapo wanafunzi 256 walifaulu kujiungana vyuo vikuu.