- 5,719 viewsDuration: 3:04Watu sita wa familia moja wamefariki kufuatia ajali iliyotokea baada ya gari walimokuwa wakisafiria kutumbukia ndani ya Mto Kiama kaunti ya Murang’a. Familia hiyo ilikuwa ikirejea nyumbani kutoka sherehe ya kulipa mahari maeneo ya Kiambu. Ajali hiyo inafikisha idadi ya waliofariki kwenye barabara katika kipindi cha saa ishirini na nne pekee kufikia watu 12.