Aliyekuwa kamanda wa polisi Nairobi atoa ushahidi wa mauaji ya Rex Masai

  • | Citizen TV
    6,986 views

    Vikao vya kesi ya mauaji dhidi ya kijana Rex Masai wakati wa maandamano ya vijana wa Gen Z vimeendelea siku ya pili huku aliyekuwa mkuu wa polisi Nairobi Adamson Bungei akijitenga kufahamu lolote kuhusu mauaji hayo. Bungei anasema hakuna risasi ya kikosi chake iliyofyatuliwa wakati wa maandamano. Aidha, afisa wa polisi aliyehusishwa na mauaji ya Rex Isaiah Muraguri naye akipata wakati mgumu kujitenga na mauaji haya