Wizara ya afya yatangaza mipango ya kurudisha programu za ukimwi, malaria, na kifua kikuu

  • | K24 Video
    18 views

    Wizara ya afya imetangaza mipango ya kurudisha programu za ukimwi, malaria, na kifua kikuu katika huduma za afya za kawaida kama hatua muhimu ya kuziba pengo la ufadhili, baada ya marekani kusitisha ufadhili kwa mataifa tofauti kwa muda. Waziri wa afya Deborah Barasa amesisitiza kuwa programu hizo tatu kuu zitasaidiwa kupitia mpango wa Taifa Care. Tangazo hilo linafuatia uamuzi wa shirika la usaid kuwapa likizo bila malipo wafanyikazi wake wote wa kimataifa kuanzia ijumaa wiki hii.