Afueni kwa wafanyikazi USAID: Baadhi ya wafanyikazi homa bay warejea kazini

  • | Citizen TV
    1,181 views

    Ni afueni kubwa kwa baadhi ya wafanyakazi waliokuwa wakifanya kazi chini ya miradi ya afya nchini inayofahdiliwa na serikali ya marekani baada ya Utawala wa Rais Donald Trump kutangaza kurejeshwa kwa muda kwa baadhi ya miradi inayookoa maisha. Zaidi ya wahudumu wa afya 560 katika Kaunti ya Homa Bay ambao walikuwa wameagizwa kusalia nyumbani wametakiwa kurejea kazini kutoa huduma muhimu za kudhibiti kusambaa kwa virusi vya HIV na matibabu yake.