Tasnia ya uanahabari nchini inaomboleza kifo cha mtangazaji mashuhuri Mambo Mbotela

  • | K24 Video
    159 views

    Tasnia ya uanahabari inaombolezwa kifo cha mtangazaji mashuhuri mkongwe katika taifa la Kenya. Sauti ambayo kwa zaidi ya nusu karne iliwahabarisha, kuelimisha, na kutangaza mengi ya kuaminika haiko tena. Mwanahabari mkongwe na mtangazaji mashuhuri, Leonard Mambo Mbotela, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 84 baada ya kuugua kwa muda.