Maafisa 144 wa polisi wamewasili Haiti kujiunga na kikosi kilichotangulia katika taifa hilo

  • | K24 Video
    201 views

    Maafisa 144 wa polisi wamewasili haiti kujiunga na kikosi kilichotangulia katika taifa hilo kusaidia kupambana na magenge ya uhalifu na kurejesha amani. Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen aliwaaga maafisa hao ambao ni kundi la tatu kuondoka nchini baada ya vikosi viwili kutangulia haiti mwaka jana na mapema mwaka huu. Hii inawadia huku rais william ruto akijitokeza na kusema kwamba taifa la marekani litaendelea kuunga mkono juhudi za kuleta uthabiti haiti baada ya taifa hilo kutangaza kusitisha ufadhili wa kigeni.